[male
vocals] 1.
Nikasikia
sauti
kubwa
kutoka
katika
kile
kiti
cha
enzi
ikisema,
Tazama,
maskani
ya
Mungu
ni
pamoja
na
wanadamu,
naye
atafanya
maskani
yake
pamoja
nao,
nao
watakuwa
watu
wake.
Naye
Mungu
mwenyewe
atakuwa
pamoja
nao.
Naye
atafuta
kila
chozi
katika
macho
yao,
wala
mauti
haitakuwapo
tena;
wala
maombolezo,
wala
kilio,
wala
maumivu
hayatakuwapo
tena;
kwa
kuwa
mambo
ya
kwanza
yamekwisha
kupita. “
Tunalo
tumaini
hili
kama
nanga
ya
roho,
imara
na
thabiti.”
Mambo
ya
kwanza
yanayo
tuumiza
yatapita
na
Mungu
mwenyewe
atakuwa
pamoja
nasi.
Mambo
yote
mapya,
Tumaini
linaanzia
hapa,
Tumaini
linaanzia
hapa. 2.
Mpendwa
ninakutia
moyo
shikilia
Imani
na
ishi
sawasawa
na
mapenzi
ya
Mungu,
ili
tuweze
kuwepo
pale,
mahali
ambapo
hakuna
kifo.
Hakuna
maombolezo.
Hakuna
maumivu.
Mungu
mwenyewe
akiwa
pamoja
nasi
na
kutufuta
machozi
yetu
kwa
mara
ya
mwisho
kabisa.
Ikiwa
umewahi
kuugua
sana,
au
kushika
mkono
wa
mpendwa
wako
aliyekuwa
katika
maumivu
makali
mwishoni
mwa
maisha
yake;
ikiwa
umewahi
kupitia
uchungu
mwingi
wa
nafsi,
au
kupambana
na
uraibu,
au
unapitia
wakati
mgumu
na
manyanyaso
makali;
usikate
tamaa
Yesu
anakuja
tena. “
Tunalo
tumaini
hili
kama
nanga
ya
roho,
imara
na
thabiti.”
Mambo
ya
kwanza
yanayo
tuumiza
yatapita
na
Mungu
mwenyewe
atakuwa
pamoja
nasi.
Mambo
yote
mapya,
Tumaini
linaanzia
hapa,
Tumaini
linaanzia
hapa!