[female vocals] Mume
wangu
Kipenzi
Patrick
Tuva,
hadithi
yetu
ya
Mapenzi
ilianza
zamani
ulipokuja
kwetu
Taita
ukanioa
na
kunipeleka
kwenu
Gongoni,
tuliishi
vyema
kwa
upendo
na
Mungu
akatubariki.
Ulipougua
mume
wangu
nilikuuguza
kwa
upendo,
hata
uliponituma
kuenda
Nairobi
kumangalia
kitinda
mimba
wetu
aliyekuwa
mgonjwa
sikujua
ilikuwa
kwa
heri,
kifo
chako
Cha
ghafla
kiliniumiza,
ijumaa
hiyo
ya
tarehe 20
mwezi
wa
pili
haitaondoka
mawazoni.
Mkeo
mimi
Edda
umeniwachia
pengo
kubwa
moyoni,
umewacha
wanao
na
wajukuu
wako
uliowapenda
sana,
mbona
mume
wangu?
Uliwacha
kanisa
lako
Victoria
Baptist
ulilolipenda
sana,
sasa
jukumu
hilo
limebaki
kwangu.
Moyo
wangu
unaniuma
kwa
kuku
kumbuka
lakini
najua
umeenda
pahali
pema
zaidi.
Nguvu
zako
za
kiroho
na
upendo
wako
vinaendelea
kuishi
ndani
yangu,
sasa
ninajukumu
la
kuendeleza
huduma
yako.
Mungu
aliyeruhusu
haya
ataniwezesha
kusimama
kwa
sababu
si
jambo
rahisi,
wakati
mwingine
mambo
hunilemea
lakini
tegemeo
langu
ni
kwa
Mungu
tu.
Mkeo
Edda
nasema,
endelea
kupumzika
kwa
Amani
mume
wangu,
rafiki
yangu,
baba
wa
watoto
wangu,
Babu
wa
wajukuu
wangu,
Bishop
wangu,
nilikupenda
lakini
Mungu
alikupenda
zaidi,
wacha
Mungu
anifariji
pamoja
na
jamii
uliyoniwachia,
bado
nakupenda
mume
wangu
Patrick
Tuva.